A Zeno.FM Station Tetesi za Soa Ulaya Ijumaa: Arsenal, Spurs zamtaka Eze

Tetesi za Soa Ulaya Ijumaa: Arsenal, Spurs zamtaka Eze


Eberechi Eze

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Eberechi Eze

Arsenal inapigana vikumbo na wapinzani wao wa Kaskazini mwa London, Tottenham katika mbioz za kumsajili kiungo wa Crystal Palace na England, Eberechi Eze, 26, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 68 (Sun).

Washika bunduki 'The Gunners' wanamsaka Eze ambaye ni mbadala wa mshambuliaji wa Real Madrid kutoka Brazil, Rodrygo, 24 anayeonekana kuwa ghali kumpata. (Talksport)

Tottenham wameweka bei ya zaidi ya pauni milioni 60 kumuuza beki wa kati wa Argentina, Cristian Romero, 27, na hawataki kumuuza kwa bei nafuu kwenda Atletico Madrid. (Telegraph)

Napoli na Juventus wako tayari kuilipa Manchester United pauni milioni 25 kwa ajili ya kumsajili Jadon Sancho, 25, lakini hawawezi kukidhi mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki wa winga huyo wa England (Metro)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Jadon Sancho

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Paris St-Germain na Ufaransa, Warren Zaire-Emery, 19 (Teamtalk),

Fulham hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 24, Rodrigo Muniz, licha ya kupigiwa simu na Leeds. (Sky Sports)

Liverpool wamefungua mazungumzo na Crystal Palace kuhusu mkataba wa kumsajili nahodha wao Marc Guehi, huku beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 24 akisemekana kupendelea kuhamia Anfield msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Newcastle wameanzisha mbio za kumsajili mshambuliaji wa Brighton kutoka Brazil, Joao Pedro, 23, kipa wa Burnley kutoka England, James Trafford, 22, na winga wa Nottingham Forest kutoka Sweden, Anthony Elanga, 23. (Telegraph)

Joao Pedro

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Joao Pedro

Kipa wa BurnleyJames Trafford amekubaliana masharti na Newcastle na mazungumzo kati ya vilabu viwili yanaendelea ili ajiunge St James Park. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamerejea katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting, Victor Gyokeres, huku mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden mwenye umri wa miaka 27 akiripotiwa kuwa tayari kuungana tena na meneja wake wa zamani Ruben Amorim huko Old Trafford. (Mirror)

West Ham wanapambana na Wolves kumsajili mshambuliaji wa Nice na Ivory Coast, Evann Guessand, 23, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25. (Mail), external

Brentford wamekubaliana kwa kiasi kikubwa mkataba wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Feyenoord mwenye umri wa miaka 20, Antoni Milambo, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi ya chini ya miaka 21. (Mirror)

Tags :-

Post a Comment

0 Comments