A Zeno.FM Station Mkataba Mpya wa Ronald ni Kufuru, Je Utawalipa AL Nassr?

Mkataba Mpya wa Ronald ni Kufuru, Je Utawalipa AL Nassr?


Ronaldo ameongeza mkataba na Al Nassr wenye thamani ya £423 Million. Hizi ni pesa nyingi sana kwa mchezaji mwenye miaka 40.

Swali ni je Al nassr watapata vipi faida kwa uwekezaji huu?

Kuongezeka Mauzo ya Ticket: Tangu ujio wa Ronaldo ndani ya Al Nassr mahudhurio yameongezeka mpaka kufikia tickets 25,000, na bei ya ticket moja ni £25. Kwa msimu Al nassr wanacheza mechi 20 so kupitia mauzo ya ticket pekee, Al nassr wana uhakika wa kutengeneza zaidi ya £12.5Millions (Billioni 40) kwa msimu, kiasi ambacho hapo awali kabla ya ujio wa Ronaldo kilikua hakiwezekani kupatikana.

Mauzo ya Jezi: Kabla ya ujio wa Ronaldo, Al Nassr walikua wanauza idadi ya Jezi 10,000 – 20,000 kwa msimu. Ujio wa Ronaldo, ushawishi wake, na wingi followers wake Instagram umeongeza mauzo ya jezi mpaka kufikia jezi 100,000 kwa msimu. Al nassr ambao wanauza jezi 1 sawa na £80 wana uhakika wa kupata £8 Millions ( Zaidi ya B19 kwa msimu)

Kuvutia wawekezaji: Uwepo wa Ronaldo, Ushawishi wake, na namna anavyofuatiliwa inavutia wawekezaji kuwekeza kwenye klabu ya Al Nassr kwa kuwa Ronaldo anaongeza namba ya watu wanaofuatilia klabu hiyo hvyo kupelekea big brands kuonekana zaidi (Brand visibility). Nike na brands zingine zimewalipa Al nassr zaidi ya Bilioni 55 kwa mwaka kupitia brands zao kuhusika na Al nassr x Ronaldo

Mapato ya TV: Kabla ya Ujio wa Ronaldo, Ligi ya Saudi Arabia ilikua inaonekana na kufuatiliwa na nchi 50 pekee. Baada ya Ronaldo kusaini, Ligi imekua inafuatiliwa na nchi zaidi ya 140. Hii imepelekea mapato ya TV kuongezeka kutoka Dola milioni 10 mpaka Dola milioni 100 kwa msimu.

Nimeongelea kwa ufupi maeneo machache tu, Ila Yapo maeneo mengi ambayo Al Nassr na ligi ya Saudi inapata faida kutokana na uwepo wa the ‘The Goat’ Cristiano Ronaldo. Mfano, Kuongezeka kwa Utalii, kushawishi wachezaji wengine wakubwa kucheza Saudi na kuwezesha Saudi kushinda nafasi ya kuandaa World cup mwaka 2030

Wenzetu kwenye suala la uwekezaji wanafikiria mbali na pesa inarudi. Je ni wakati sahihi na sisi tumtumia Samatta kama balozi wa NBC PREMIER LEAGUE?

Tags :-

Post a Comment

0 Comments