
BREAKING: Eng Hersi wa Yanga Achukua Form ya Ubunge Kigamboni
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, leo Juni 28, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hersi ambaye amepata mafanikio makubwa katika uongozi wake akiwa na klabu ya Yanga ikiwemo ubingwa wa ligi mara nne mfululizo sasa anahamishia nguvu zake kwenye siasa akilenga kulitumikia taifa kwa nafasi nyingine.