
Basata Waifungia Kampuni Inayoendesha Mashindano ya Miss Tanzania
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeiondolea sifa kampuni inayoendesha mashindano ya Miss Tanzania kutokana na Kushindwa kuhuisha kibali cha kufanya kazi za sanaa kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila sababu ya msingi na pia kukaidi agizo halali la Baraza la kuwasilisha nyaraka hususani nakala ya cheti/leseni ya kushiriki shindano la urembo wa Dunia, pamoja na Kushindwa kufanya shindano la urembo kwa mwaka 2023/2024 na kushindwa kumpeleka Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la urembo wa Dunia kwa mwaka 2024/2025 bila sababu za msingi.
Maamuzi yote hayo yametokana na ukiukwaji wa kanuni ya 39 (g na f) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018, hivyo Baraza limefikia uamuzi wa kumuondolea sifa za kuendesha shindano la Miss Tanzania na kwamba kwa mujinu wa sheria kampuni hiyo ina haki ya kukata rufaa kwa Waziri husika.