Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Mo Salah anataka kwenda Uarabuni - IDDYNATION SITE

Breaking News

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Mo Salah anataka kwenda Uarabuni

 

a

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Mo Salah

Kuna imani kubwa nchini Saudi Arabia kwamba mshambuliaji wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 32, yuko tayari kujiunga na ligi kuu ya nchi hiyo (Saudi Pro League) mara tu mkataba wake na The Reds utakapomalizika msimu huu wa joto.

Manchester United wameongeza juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Ipswich, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anathamani ya £40m. (Mail)

Newcastle wanaendelea kuonyesha nia ya kumsajili kipa wa Burnley, James Trafford, mwenye umri wa miaka 22, msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Kiungo wa Ureno, Bernardo Silva, mwenye umri wa miaka 30, anataka kuondoka Manchester City msimu huu wa joto ili kutafuta changamoto nje ya Liki kuu ya England (Football Insider).

Bernardo Silva

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Bernardo Silva

Brighton wameweka bei ghali ya £100m kwa ajili ya mshambuliaji wa Mbrazil Joao Pedro, mwenye umri wa miaka 23, na kiungo wa Cameroon Carlos Baleba, mwenye umri wa miaka 21, ili kuzuia nia ya Liverpool, Newcastle, na Chelsea zinazotaka kuwasajili (Talksport).

Arsenal, Newcastle, Chelsea, na Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anatarajiwa kuondoka Juventus msimu huu wa joto. (Gazzetta dello Sport)

Newcastle wanapanga mpango wa kushtukiza wa kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool, Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 21. (Teamtalk)

Dusan Vlahovic

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Dusan Vlahovic

Chelsea wanatafakari uwezekano wa kutoa ofa ya thamani ya euro 40m (£33.4m) kwa ajili ya mshambuliaji wa Villarreal, Thierno Barry, mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ufaransa. (Fichajes)

Arsenal, Newcastle, na Nottingham Forest ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na beki wa Roma kutoka Ivory Coast, Evan Ndicka, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ana thamani ya euro 40m (£33.4m). (Caught Offside).

Kocha wa Crystal Palace, Oliver Glasner, bado anawania kuchukua nafasi ya kuinoa RB Leipzig msimu ujao baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 50. (Sky Germany)

Crystal Palace wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ufaransa, endapo mshambuliaji mwenzake wa Kifaransa, Jean-Philippe Mateta, mwenye umri wa miaka 27, ataondoka klabuni msimu huu wa joto. (Teamtalk)

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.