Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City yamtaka Saliba, Ronaldo aikataa Inter - IDDYNATION SITE

Breaking News

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City yamtaka Saliba, Ronaldo aikataa Inter

 

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Saliba

Manchester City wanapanga kumsajili beki wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, William Saliba, katika majira ya joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia anawindwa na Real Madrid.

Kiungo wa AC Milan na timu ya taifa ya Uholanzi, Tijjani Reijnders, mwenye umri wa miaka 26, pia ni lengo la Manchester City, ambao tayari wamewasiliana na klabu ya Serie A.

Bournemouth wanataka pauni milioni 45 kwa beki wa kushoto wa Serbia, Milos Kerkez, mwenye umri wa miaka 21, huku Liverpool wakionyesha nia ya kumsajili.

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Ronaldo

Uwezekano wa mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 40, Cristiano Ronaldo, kujiunga na Inter Milan kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu hauchukuliwi kwa uzito na klabu hiyo ya Serie A.

Arsenal wanamzingatia mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 22, kama mbadala wa mfungaji wa Newcastle, Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25.

Chelsea kwa sasa hawatarajii kusajili kipa mpya wa kikosi cha kwanza majira ya joto. Kocha wa The Blues, Enzo Maresca, ataachia ushindani kati ya Djordje Petrovic, mwenye umri wa miaka 25, ambaye yuko kwa mkopo Strasbourg, na Mike Penders, kipa wa miaka 19 kutoka Genk.

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Bukayo Saka

Winga wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Bukayo Saka, ataingia katika mazungumzo mapya ya mkataba, huku mkurugenzi mpya wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, akitaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 asaini mkataba wa muda mrefu.

Barcelona wameeleza kuwa kiungo wao wa Uhispania, Pedri, mwenye umri wa miaka 22, hayupo sokoni licha ya uvumi kwamba Manchester City wanamtaka kama mbadala wa Kevin De Bruyne.

Fabio Paratici, aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa Tottenham, anatarajiwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa AC Milan mwezi Juni, baada ya marufuku yake ya shughuli za soka nchini Italia kumalizika.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.