Yanga SC imetoa siku za mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union. Kikosi cha Young Africans kitarajea mazoezi siku ya Jumatano Machi 29 kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Tabora United utakaopigwa April 1 pale Tabora.
Wananchi, Young Africans SC wametinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Wanamangushi, Coastal Union katika uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam