VIONGOZI WA DINI NCHINI SPAIN WAMRUHUSU LAMINE YAMMAL KUTOFUNGA SIKU ZA MECHI ILI KULINDA AFYA YAKE KUTOKANA NA UMRI WAKE ALIONAO - IDDYNATION SITE

Breaking News

VIONGOZI WA DINI NCHINI SPAIN WAMRUHUSU LAMINE YAMMAL KUTOFUNGA SIKU ZA MECHI ILI KULINDA AFYA YAKE KUTOKANA NA UMRI WAKE ALIONAO


Ofisi kuu ya baraza la dini ya kiislamu nchini Spain limetoa idhini ya Mchezaji kinda wa klabu ya FC Barcelona raia wa Spain Lamine Nasroui Yammal Ebana kutofunga swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani siku ambazo timu yake Ina mechi na mpaka muda wa mechi unafikia,muda wa kufungua unakuwa bado haujafika.
Sababu kuu ya baraza hilo kumruhusu ni Kwa ajili ya kulinda afya yake ya mwili kutokana na kazi anayofanya,Lamine Yammal ana umri wa miaka 17 Bado mdogo sana kiafya kuweza ku maintain energy akiwa hana kitu tumboni.
Pia kitabibu Bado nutritional balance yake haiko sawa na mtu mwenye umri kuanzia miaka 20 na kuendelea.
Wataalamu wa afya katika idara ya FC Barcelona waliwasilisba taarifa kwenda Baraza la dini ya kiislamu wakisema kuwa, Lamine Nasroui Yammal Ebana Kucheza mpira akiwa amefunga yaweza msababishia kuishiwa nguvu hali inayoweza kupelekea akapoteza fahamu akiwa ndani ya pitch.
Kwahiyo kijana hatotakiwa kufunga kwa siku ambazo timu yake itacheza mechi muda ambao mpaka mechi inaanza wakati wa kufuturu unakuwa bado tu.
Lakini kama mechi itakuwa usiku baada ya wakati wa kufuturu,basi Lamine Yammal atatakiwa kufunga siku hiyo.
Pia siku ambazo hatofunga kwa dharula hiyo atazilipa baadae mwezi Ramadhani utakapomalizika.
Source: [ Diario AS ]


 

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.