A Zeno.FM Station Tetesi za soka Ulaya: Viktor Gyokeres 'lulu' mpya Ulaya

Tetesi za soka Ulaya: Viktor Gyokeres 'lulu' mpya Ulaya

IDDY AMAN
0

Liverpool, Manchester City au Arsenal zitakuwa timu anazozipendelea Viktor Gyokeres iwapo mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 ataondoka Sporting msimu huu wa joto. (A Bola)

Bayern Munich na Real Madrid wana nia ya kutaka kumnunua beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 25. (Teamtalk)

Liverpool wanafikiria kumnunua beki wa Borussia Dortmund wa Ujerumani Nico Schlotterbeck, 25, ambaye wanamwona kama mbadala wa muda mrefu wa Virgil van Dijk. (Bild)


Arsenal wako katika nafasi nzuri mbele ya Barcelona kumsajili mlinda lango wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 23. (Cadena Ser)

Manchester United wanaweza kumnunua Dusan Vlahovic huku Juventus wakiwa tayari kupunguza bei yao ya £35m kwa mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 25. (Givemesport)

Tottenham wameanza mazungumzo na Angel Gomes kuhusu uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza Lille, 24, itakapokamilika msimu huu wa joto. (Football transfers)

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa umri wa chini ya miaka 20 wa Rosario wa Argentina Juan Gimenez. (Football Insider)

Liverpool wameanza kutafuta dili la kumnunua beki wa pembeni wa Bournemouth kutoka Hungary Milos Kerkez, 21. (Teamtalk)


Leeds wana makubaliano ya mdomo kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 29, kutoka Manchester City (Teamtalk)

Newcastle wanapanga kumnunua fowadi wa Ipswich Town Liam Delap, 22, kwa kuwa Muingereza huyo anataka kusalia katika Ligi ya Premia (Football insider)

Kinda wa Uturuki Arda Guler anataka kuondoka Real Madrid kutatizika, huku Inter Milan na AC Milan wakiripotiwa kumtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sport)

 

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default