Liverpool wamewasiliana na watu wa karibu na mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 25, kabla ya kuanza mchakato wa uhamisho wa majira ya joto. (Fabrizio Romano)
Manchester United imepandisha bei ya Marcus Rashford, 27, ambaye kiwango chake bora akiwa kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa kimemfanya aitwe tena England. (Football Insider)
Wolves wanafuatilia kwa karibu suala la Diogo Jota huko Liverpool na wanafikiria kuchukua hatua ya kumrejesha Molineux mshambuliaji huyo wa Ureno, 28, msimu huu wa joto. (Teamtalk).
Bournemouth wana uhakika wa kumsajili mlinda mlango wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 26, kutoka Liverpool msimu huu. (Sun).
AC Milan itamsajili kwa usajili wa kudumu beki wa Manchester City na Uingereza Kyle Walker, 34, msimu wa joto, lakini haitalenga kumbakisha mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 25, kwa sasa kwa mkopo kutoka Chelsea. (Gazzetta dello Sport).
Liverpool inapanga kutumia zaidi ya £250m msimu huu wa joto kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 25, kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 21, na mlinzi wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 25. (Fichajes),
Liverpool ni moja ya klabu zinazomfuatilia beki wa kulia wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, huku wakimuona beki huyo wa kulia wa Uholanzi, 24, kama mbadala wa Trent Alexander-Arnold. (Caught Offside)