
Real inamfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Hispania Nico Williams, 22, ambaye ana kipengele cha kuuuzwa kwa euro 62m (£51.8m), iwapo nyota wa Brazil Vinicius Jr, 24, atakubali uhamisho wa kitita kinono kwenda Saudi Arabia. (Fichajes)
Real Madrid inamtaka Nico baada ya kukubaliana na mlinzi wa pembeni wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, waliompa mkataba wa miaka mitano na atajiunga na wababe hao wa Uhispania bila malipo. (Sky Sports)
Manchester United inapanga kuwaruhusu wachezaji 10, akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33 - kuondoka kabisa katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)