Arsenal na Bayern Munich wako katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Uhispania Nico Williams, huku mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak akisema kuna uwezekano akazungumza na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya.
Bayern Munich wamefufua nia yao ya kutaka kumsajili winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal. (Bild)
Mshambulizi anayekodolewa macho wa Newcastle na Uswidi Alexander Isak, 25, anasema "pengine" atazungumza na klabu kuhusu mkataba mpya msimu wa joto. (Mail)
Real Madrid wanamfuatilia mlinzi wa Tottenham na Argentina Cristian Romero, 26, na mlinzi wa kati wa Everton wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22, ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Teamtalk)
Chelsea wamekubali dili la kumnunua kiungo wa kati wa Ureno chini ya miaka 21 Dario Essugo, 20, kutoka Sporting kwa pauni milioni 21, kufuatia kipindi chake cha mkopo msimu huu huko Las Palmas. (A Bola - in Portuguese)
Everton wanapanga kumsajili mshambliaji wa Morocco Hamza Igamane, 22, kutoka Rangers msimu wa joto. (Football Insider)
Liverpool itakabiliana na ushindani kutoka kwa Arsenal kumsajili winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, mkataba wake utakapomalizika Bayern Munich msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish)
Brighton wanatarajia ofa za zaidi ya pauni milioni 20 kwa kiungo wao Msweden Yasin Ayari, 21, ambaye anawindwa na Borussia Dortmund na AC Milan. (Football Insider)