A Zeno.FM Station Tetesi za Soka Ulaya: City, Man Utd zatoana roho kwa Wharton

Tetesi za Soka Ulaya: City, Man Utd zatoana roho kwa Wharton

IDDY AMAN
0


 Vilabu vya Manchester City na Manchester United vimejiandaa kupambana ili kumsajili kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, 21, majira ya kiangazi. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, hana kipingamizi kuhamia Juventus majira ya kiangazi. (Gazzetta dello Sport)

Real Madrid wanajiandaa kuingilia kati dili la Arsenal kwa kiungo wa Real Sociedad na timu ya taifa ya Hispania, Martin Zubimendi, 26, kama sehemu ya mchakato wao wa kujenga upya kikosi chao. Wana mpango pia wa kumsajili beki wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Trent Alexander-Arnold, 26, pamoja na beki wa kati wa Bournemouth na timu ya taifa ya Hispania, Dean Huijsen, 19. (AS, via Teamtalk)


Manchester United wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji, na wanamfuatilia kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Uturuki, Kenan Yildiz, 19, pamoja na mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons, 21. (Florian Plettenberg)

Arsenal watampa winga Ethan Nwaneri, 18, mkataba mpya wa miaka mitano ili kuwazuia Chelsea na Manchester City kumnyakua kiungo huyo wa kimataifa wa vijana wa England. (Mail)

Barcelona wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Hispania, Ferran Torres, 25, kwa karibu £30m, huku Aston Villa, Liverpool na Manchester United wakimfuatilia mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City. (Fichajes)


Tottenham italazimika kulipa £40m ili kumsajili beki wa Algeria, Rayan Ait-Nouri, 23, huku Liverpool, Arsenal na Manchester United pia wakionyesha nia ya kumnasa beki huyo wa Wolves. (Football Insider)

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, 52, anatajwa kuwa chaguo bora ikiwa Juventus wataamua kumfuta kazi kocha wao wa sasa, Thiago Motta, 42. Zidane aliwahi kucheza kwa miaka mitano katika klabu hiyo ya Serie A. (Gazzetta dello Sport)

Beki wa kati wa Ujerumani, Antonio Rudiger, 32, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka Real Madrid licha ya kuwaniwa na klabu inayoshiri ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League), Al-Nassr. (90min)

Nottingham Forest wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili ili kumsajili mshambuliaji wa Wolves, Matheus Cunha, 25, ambapo mchezaji huyo wa Brazil anatarajiwa kugharimu karibu £60m. (TBR Football)

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default