Tetesi kubwa 5 za soka Ulaya: Salah, Pogba, Berta, Frimpong ana Cambiaso

Mohamed Salah anaweza kuwa karibu zaidi kuliko hapo awali kufunga mustakabali wake wa Liverpool kwani ameingia kwenye mazungumzo mazito ya kuongezewa mkataba, kwa mujibu wa chombo kikuu cha Misri (skysport)
Salah anamaliza mkataba wake miezi miwili na nusu ijayo na Liverpool wanajaribu kumbakiza, huku yeye akicheza turufu muhimu ya kupata mkataba wa maana zaidi kwa kuwa pengine utakuwa mkataba wake mkubwa wa mwisho katika maisha yake ya soka.

Liverpool wanaripotiwa kufanya mazungumzo ya awali kuhusu usajili wa Jeremie Frimpong na 'The Reds' wanatakiwa kutoa pauni milioni 50 huku wakikabiliwa na upinzani kutoka kwa Man City. Liverpool wanataka pia kumnunua nyota wa Juventus, Andrea Cambiaso wakihaha kuziba nafasi ya Trent Alexander-Arnold anayetimkia Real Madrid (SKysport).

Klabu ya Bayern Munich imethibitisha kuwa katika mazungumzo ya kuongeza mikataba mipya kwa wachezaji wake nyota watatu.
Mkongwe Thomas Muller, Winga Leroy Sane na kiungo `Eric Dier, wako katika nyakati za mwisho za mikataba yao na Bayern inaona wanao mchango wa kuisaidia Klabu hiyo kuendelea kutamba katika ligi kuu ya Ujerumani na mabingwa Ulaya (Romano)

Rais wa Marseille, Pablo Longoria ameeleza ni kwa nini klabu yake ilichagua kutomsajili Paul Pogba katika dirisha la majira ya baridi kali - kwa sababu ilifikiriwa kuwa "muda wake wa kupona na kutoka kwenye matatizo yake ungeweza kuvuruga utulivu wa kikosi" (Daily Mail)
Berta kutangazwa lini Arsenal?
Arsenal inakaribia kumtangaza mkurugenzi wake mpya wa ufundi, Andrea Berta.
Kila kitu kimeshakamilika kilichobaki sasa ni siku tu ya kutangazwa kwa Berta anayechukua nafasi ya Edu aliyejiondoa miezi michache iliyopita.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, amekwisha saini mkataba karibu siku 20 zilizopita (Romano)
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.