'Dini kwanza kabla ya soka', maisha ya wanasoka kwenye mfungo wa Ramadhani - IDDYNATION SITE

Breaking News

'Dini kwanza kabla ya soka', maisha ya wanasoka kwenye mfungo wa Ramadhani

 

Dango Ouattara aliyevalia jezi nyekundu na nyeusi za Bournemouth akipiga magoti kwenye uwanja wa mpira,  huku paji lake la uso likigusa nyasi.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Dango Ouattara huswali kabla na baada ya kila mchezo anaocheza, pamoja na maombi yake ya mara tano kila siku
  • Author,Ian Williams
  • Nafa

''Kwangu mimi, nimeipa dini yangu kipaumbele. Na ya kwanza kabla soka.''

Mshambuliaji kutoka taifa la Burkina Faso ni muumini wa dini ya kiislamu ambaye hufanya maombi mara tano kwa siku, kabla na baada ya mechi anazozicheza, akisema humsaidia kuishi ''na unyenyekevu''.

''Hunifanya mimi kujitathmini na kurejea kwa mola wangu, ambayo hujipima nilichofanya vizuri na nilichokosea,'' mwanasoka huyo wa miaka 23 aiambia BBC alipokuwa akifanya ibada katika msikiti ulioko Poole.

"Pia inaturuhusu kujisahihisha katika jamii pia. Inaturuhusu kukaa kwenye njia sahihi.

Wakati wa mazungumzo, Ouattara amependelea kutumia maneno kama ''utulivu'' na ''uthabiti'' kuelezea umuhimu wa dini ya kiislamu.

Mwanasoka huyo ambaye ana sifa bainifu, akionekana mwenye haya, ambaye hana matashtiti mengi.

Akiwa amefika mapema kwa mahojiano yetu naye, akiwa amevalia nguo nyeupe anatuomba tumpe muda afanye ibada kabla ya kikao chetu.

''Imani yangu uniruhusu kukabiliana na changamoto nyingi za maisha, kuheshimu watu, na pia kikubwa zaidi kuheshimu maamuzi na dini za wengine,'' anaelezea.

''Nikiwa uwanjani, nikitangamana na familia pamoja na marafiki, imani yangu hunifanya nikawa mtulivu katika maisha yangu ya kila siku.

''Unapaswa kuamini kabla ya kufanya jambo.''

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.