MAREKANI WAITHIBITISHA REMDESIVIR KUTIBU CORONA: Mamlaka za Marekani zimethibitisha dawa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona inayojulikana kama remdesivir kuanza kutibu wagonjwa wa Covid-19 katika hospitali nchini humo.
Hata hivyo Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo imeitaja pia dawa aina ya Veklury, kuwa dawa iliyoonesha uwezo wa wastani wa kuponesha kwa siku tano wakati wa majaribio..
"Veklury ndiyo ilikuwa tiba ya kwanza kutibu Covid-19 ambayo ilipokelewa na kuthibitishwa na FDA," imesema sehemu ya taarifa ya FDA.
Aidha kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) juma lililopita limesema remdesivir imekuwa haina madhara kwa wagonjwa manusura waliofanyiwa majaribio.
WHO imesema katika utafiti wao wamebaini uwezo wake daw ahiyo na kuongeza kuwa dawa iliyotengenezwa na Gilead ilikataliwa kufuatia majaribio yake.
Remdesivir ilithibitishwa na mamlaka za nchi hiyo kutumika kwa dharura na ndani ya Marekani pekee tangu mwezi Mei.
Hivi karibuni, Rais Donald Trump alipewa dawa hiyo baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya Covid-19 na kisha kutangaza amepona kabisa.
Katika taarifa yao FDA wamesema, dawa hiyo imethibitishwa jana Alhamisi “kwaajili ya matumizi ya watu wazima, wagonjwa watoto wenye umri wa miaka 12, wazee watakaokuwa na uzito wa angalau kilogramu 40 ".
Jumla ya dawa Nne zilifanyiwa majaribio kwa watu wazima takribani 11,266 katika hospitali 500 na katika nchi tofauti zaidi ya 30.
#remdesivir #Covid19 #DonaldTrump #Corona #Marekani #dawa #hospitali #matibabu