Mpenzi mpya wa Rihanna ni bilionea wa Toyota
Mapema
wiki hii picha zinazomwonyesha mwanamuziki Rihanna akiwa ndani ya bwawa
la kuogelea na mwanamume wa Kiarabu zilizagaa mitandaoni.Hatimaye
Rihanna ametoka hadharani na mwanamume huyo na ametambulika kuwa ni
bilionea wa magari ya Toyota nchini Saudia Arabia, Hassan Jameel.
Mwanamume
huyo ni makamu wa Rais wa Kampuni ya familia yake iitwayo Abdul Latif
Jameel Domestic ambayo imepewa leseni ya kuuza magari yanayotengenezwa
na Kampuni ya Toyota nchini Saudi Arabia tangu mwaka 1955.Jarida la
Forbes mwaka jana liliitaja familia ya Jameel kushika namba 15 katika
orodha ya matajiri katika nchi za Mashariki ya Kati.
jameel
pia anamiliki ligi ya mpira wa miguu nchini Saudi Arabia maarufu kama
Jameel League.Mwanamume huyo pia siyo mgeni katika viwanja vya watu
maarufu nchini Marekani, mwaka jana aliwahi kutajwa kuwa ana uhusiano wa
kimapenzi na mwanamitindo maarufu Naomi Campbell.
Rihanna
kabla ya kutua kwa Mwarabu huyo amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na rapa Drake naTravis Scott, mcheza kikapu Matt Kemp na mwimbaji waR&B,ChrisBrown.


No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.