Tetesi za soka : Wissa anapendelea kuhamia Tottenham
Mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa angependelea kumfuata meneja wa zamani wa Bees Thomas Frank kwenda Tottenham, licha ya Newcastle United kuonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), 28. (Talksport)Everton wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz kutoka Juventus, huku Aston Villa na West Ham pia zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (TeamTalk)
Arsenal walimnunua kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 30, mapema msimu huu lakini hawakuweza kuafikiana na Bayern Munich. (Bild - in Germany)
Wolves wamekubali mkataba wa kumsaini winga wa Colombia Jhon Arias, 27, kutoka klabu ya Fluminense ya Brazil. (ESPN)