A Zeno.FM Station Harmonize Afunguka Tetesi za Kuwania Ubunge Tandahimba “Bado Nahitaji Grammy”

Harmonize Afunguka Tetesi za Kuwania Ubunge Tandahimba “Bado Nahitaji Grammy”


Harmonize amevunja ukimya kuhusu safari yake ya kisiasa kwa mara nyingine tena. Kupitia posti yake ya Instagram leo Juni 30, 2025, Harmonize ameeleza wazi kuwa hatagombea tena ubunge wa Tandahimba, licha ya kuwa aliwahi kuonesha nia hiyo miaka ya nyuma akihamasishwa na Hayati Rais John Magufuli.

Katika maneno yake, Harmonize amesema hawezi kuwa sehemu ya siasa kwa sasa kwani hawezi kuacha kusema mambo kwa uhuru wake wa kisanii. Ameandika:

“Simuoni KONDEBOY kwaninyavyoona hata kusema BOMBOCLAATY sitoruhusiwa… Tandahimba chaguani kiongozi bora atakayemsaidia Rais wetu miaka 5 ijayo… Am hungry for the Grammy & more success.”

Kauli hiyo inaonesha kuwa msanii huyo bado ana ndoto kubwa za kimataifa na anaelekeza nguvu zake kwenye muziki na mafanikio ya juu kama tuzo za Grammy.

Swali: Tumchukulie Harmonize kama msanii aliyekwepa jukumu la kisiasa, au kama mtu mwenye hekima aliyetambua nafasi yake sahihi? Katika kizazi hiki cha wasanii wenye ushawishi mkubwa, nafasi yao katika uongozi bado ni hoja inayohitaji tafakuri ya kina.

Post a Comment

0 Comments